Ruka hadi yaliyomo

Shirika Lako

Shirika lako limechagua kufanya zana ya mawasiliano ya SpeakUp® iliyotengenezwa na kampuni ya People Intouch B.V. (‘sisi’, ‘nasi’, ‘yetu’) ipatikane kwako.

Kampuni ya People Intouch B.V. inapatikana nchini Uholanzi, katika Umoja wa Ulaya (EU), na kwa hiyo tumejitolea kufuata kanuni ya GDPR ya EU (Kanuni ya Jumla ya Ulinzi wa Data), ambayo ni mojawapo ya kanuni za kina zaidi za ulinzi wa data ya binafsi duniani.

Taarifa hii ya Faragha inakuhusu unapotumia programu ya SpeakUp® kuwasiliana na Shirika lako.

Kuhusu Programu ya SpeakUp®

Kupitia programu ya SpeakUp®, unaweza kuwasilisha ripoti na kuanzisha mazungumzo salama na Shirika lako ndani ya programu ya SpeakUp®.

Shirika lako linawajibika kwa uchakataji wa data yako ya binafsi kupitia programu ya SpeakUp® na ndilo linalodhibiti data. Ikiwa una maswali yoyote kuhusu programu ya SpeakUp® na jinsi data yako ya binafsi itakavyochakatwa, tafadhali wasiliana na Shirika lako au soma Sera yake ya programu ya SpeakUp na/au Sera ya Faragha. Kampuni ya People Intouch ndiyo inayochakata data, na tunachukulia jukumu hilo kwa uzito sana. Hii inamaanisha kwamba tunakupa njia salama zaidi kadri iwezekanavyo ya kuwasiliana na Shirika lako.

Faragha yako ni muhimu kwetu. Tunataka ujihisi salama unapotumia programu ya SpeakUp® na tungependa kukujulisha kuhusu yafuatayo:

Data nyeti

Programu ya SpeakUp® haikusudiwi kuwasilisha data nyeti ya binafsi kama vile asili, data ya afya, mitazamo ya kisiasa, imani za kifalsafa (za kidini au ukanaji Mungu n.k.), mwelekeo wa kuvutiwa kimapenzi au historia ya kisheria. Tunakuomba uzingatie hili unapotumia programu ya SpeakUp®.

Watoto wadogo

Ikiwa wewe ni mtoto mdogo, Shirika lako litahitaji kupata idhini kutoka kwa wazazi au walezi wako ili uweze kutumia programu ya SpeakUp®, ikiwa inahitajika kisheria.

Jinsi inavyofanya kazi

Je, itakuwaje kwa ripoti inayowasilishwa kupitia programu ya SpeakUp®?

Maudhui ya ripoti hiyo hushirikiwa na Shirika lako na yatatumiwa na kuchakatwa tu kwa madhumuni ambayo programu ya SpeakUp® inakusudiwa na Shirika lako. Ripoti hushirikiwa kila wakati na Shirika lako kwa njia ya maandishi. Ripoti za sauti hunakiliwa kabla ya kushirikiwa, na faili ya sauti hufutwa kiotomatiki. Unaweza kuwasha taarifa za barua pepe au arifa za programu ya SpeakUp®. Unaweza kuzima arifa za programu ya simu ya mkononi ya SpeakUp® wakati wowote kupitia mipangilio ya kifaa chako. Soma Sera ya Shirika lako ya programu ya SpeakUp na/au Sera ya Faragha kwa maelezo zaidi kuhusu kinachotokea kwa ripoti inayowasilishwa kupitia programu ya SpeakUp®.

Kutotambulika

Unapowasilisha ripoti kupitia programu ya SpeakUp®, unaweza kuamua kujitambulisha kwa Shirika lako au kutojitambulisha. Ukishiriki maelezo ya binafsi kwenye ripoti yako, haya yatachakatwa na Shirika lako linaposhughulikia ripoti yako.

Kwa nini data ya binafsi huchakatwa wakati wa kutumia programu ya SpeakUp®?

Uchakataji wa data ya binafsi kupitia programu ya SpeakUp® ni muhimu:

Je, ni data gani ambayo huchakatwa?

Data fulani unayotoa hukusanywa kiotomatiki unapotumia programu ya SpeakUp® na haitashirikiwa na Shirika lako. Data hii huchakatwa ili kukupa huduma ya vipengele vyote vya programu ya SpeakUp®, kwa madhumuni ya uthibitishaji, kwa madhumuni ya kutuma arifa (ikiwashwa; k.m. anwani yako ya barua pepe), ili kuanzisha muunganisho salama na kifaa chako na kuzuia na kugundua hatari za usalama au shughuli zingine hasidi. Maelezo haya hayatatumiwa kamwe kwa madhumuni mengine yoyote na yatahifadhiwa tu kwa muda unaohitajika kwa madhumuni yaliyokusudiwa, isipokuwa muda huu uongezwe kwa sababu ya kitendo hasidi kilichotambuliwa.

Usalama wa data

Kampuni ya People Intouch imechukua hatua za kina ili kuzuia kupotea, matumizi mabaya au ubadilishaji wa data yako ya binafsi. Data yote husimbwa kwa njia fiche inapotumwa kupitia wavuti ya shirika la SpeakUp® na programu ya simu ya mkononi ya SpeakUp®. 

Vidakuzi

Unapotembelea wavuti ya SpeakUp®, vidakuzi vya kipindi hutumiwa kutoa mawasiliano salama. Data ya kidakuzi hiki cha kipindi itafutwa baada ya saa mbili (2). Unaweza kutumia mipangilio ya kivinjari chako kufuta, kuzima au kuzuia vidakuzi.

Marekebisho

Kampuni ya People Intouch ingependa kuendela kukupa taarifa kwa njia bora zaidi kadri iwezekanavyo, na inaweza kurekebisha na kubadilisha Taarifa hii ya Faragha mara kwa mara.

Haki zako ni zipi?

Shirika lako linawajibika kwa uchakataji wa data yako ya binafsi na kukuhakikishia haki zako zinazotokana na sheria zinazotumika za ulinzi wa data. Tafadhali soma Sera ya programu ya SpeakUp na/au Sera ya Faragha ya Shirika lako kwa maelezo zaidi kuhusu uchakataji wa data ya binafsi na Shirika lako na haki zako za ulinzi wa data.

Ilirekebishwa mara ya mwisho tarehe 12 Julai 2022

***